WAJASIRIAMALI 30 WAPIGWA MSASA NA SHIRIKA LA TYC SHINYANGA
“Tumeamua kuendesha mafunzo haya kwa sababu tunao watu ambao ni wanufaika wa mradi wa ‘Soap Making Project’ kwa ufadhili wa Shirika la Tanzania Development Trust(TDT) ambao unatelelezwa hapa manispaa na tumedhamiria kuendesha mafunzo haya ili kuimarisha biashara zao,ufungashaji na namna ya kuendesha biashara na sisi tumegundua ya kwamba ni lazima tuhuishe mafunzo yao na wafundishwe namna ya kufanya biashara kwa ubora zaidi kwenye mitaa na hata nje ya mkoa wa Shinyanga” amesema Bw.Maganga